News: CHAWATA wamuangukia JPM.. wataka Bajaji zao zisamehe tozo !! ..share..

CHAMA cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) wamemuomba Rais John Magufuli kuziachia Bajaji kuendeshwa na walemavu kote Nchini na kuwaondolea kodi za kuziagiza.

Mwenyekiti wa (CHAWATA) wa kwanza kushoto,John Mluba akizungumza na waandishi wa wahabari 


Pia wamesisitiza kwa kuiomba Serikali iziagize bajaji 3000 na kuwakopesha watu wenye ulemavu ili ziweze kutumia kwa ajili ya kufanya kazi kwa kutekeleza kauli ya “Hapa Kazi”na kuacha utegemea wa kuomba omba ovyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,Mwenyekiti wa (CHAWATA) Taifa, John Mlabu amesema kutokana na walemavu wengi kukosa fursa za kujiwezesha katika kukuza maendeleo ya kiuchumi hali hiyo imewasababishia baadhi yao kukosa kazi kwa kutegemea kazi ya bajaji pekee.

“Asilimia kubwa ya walemavu wanaoendesha bajaji katika eneo la Kivukoni ambalo tulilokabidhiwa na Serikali ni waajiriwa hali ambayo kwa siku tunapeleka hesabu ya shilingi 20000 kwa matajiri wetu, ufanye kazi usifanye tajiri anahitaji fedha,”Mlabu.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imekuja na mipango ya kuiweka nchi katika uchumi wa kati na ujenzi wa viwanda na wao kama sehemu ya wananchi wa Taifa hilo ili kuweza kuunga mkono jitihada za Serikali ni vema kuwawezesha walemavu kufanya kazi pia hali ambayo baadhi yao walikosa fursa hizo kutoka katika maeneo mengine ya kazi.

Aidha wamemuomba Rais Magufuli kuwaachia wazitumie bajaji nchini katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kuacha utegemezi wa kuomba barabarani.

“Tunamuomba Raisi kutuondolea tozo za kuingiza bajaji pia kutupatia fursa ya kupata mkopo wa bajaji ili tuweze kufanya kazi kwa jitihada bila wasiwasi juu ya fedha ya tajiri tunayoipeleka kila siku kwa wahusika wa vyombo hivi,”alisema Mlabu.

Amesema wanampongeza Raisi Magufuli na Serikali yake kwa kuwajali watu chini na maskini kama walemavu na kumuomba Raisi kuliangalia kundi hilo kwa jicho la pekee maana maisha ya mtu mwenye ni magumu hivyo kupata fursa ya kutumikia bajaji katika kujiwezesha kiuchumi,kutawasaidia kuwaendeleza mbele.

Na: Dalila Sharif.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search