News: STarTimes yapongezwa kwa kurahisisha upatikanaji wa TV ya kidigitali...#share
WAJUMBE kutoka kitengo cha
Usimamizi na Udhibiti wa Mawasiliano ya Kimtandao kutoka China umeipongeza
Kampuni ya Star Media Tanzania kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa TV ya digital
na kufikia uchumi wa nchi mbalimbali.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya
habari na Ofisa Uhusiano wa Star Times Josephine Stephen, ilisema Ujumbe huo
ulitoa pongezi hizo juzi walipoitembelea kampuni hiyo Makao Makuu yaliyopo
Mikocheni jijini Dar es Salaam ili kujionea jinsi inavyofanya kazi nchini
Tanzania.
Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa
kitengo hicho Zhen Cheng, alisema kuwa jitihada kubwa zilizofanywa na kampuni ya
Star Media Tanzania katika uhamiaji wa digital ni vizuri kuheshimiwa na kutoa
fursa kwa Watanzania kuendeleza na kushiriki uzoefu wao juu ya upanuzi wa
teknolojia ya digital pamoja na mipango ya baadaye.
Aidha ujumbe huo uliipongeza Star
Media kwa jinsi ilivyojiimaarisha kwa kuanzisha matawi yake na kuajiri watu
wengi nchini.
Cheng alieleza kuwa China ina nia ya
kuendeleza ushirikiano wa kina na Tanzania katika kutoa mafunzo ya kukuza na
kuendeleza wafanyakazi nchini.
“Ushirikiano kati ya China na Tanzania umekuwa mzuri tangu miaka
mingi iliyopita. China ina nia ya kuwa na ushirikiano wa kina katika mafunzo ya
kukuza, na kuendeleza wafanyakazi wa Tanzania ambao watafanya ,” alisema Cheng.
Makamu wa Rais wa kampuni ya Star
Media Carter Luo aliukaribisha ujumbe
huo na aliweza kueleza jinsi wanavyofanya kazi nchini na kufanikisha kubadilisha
familia nyingi za Tanzania kutoka maisha ya analog hadi ya digital.
Timu ya Uwakilishi huo
ilijumuisha CCTV, shirika la Xinhua na Daily Online ambapo baada ya kukamilika
kwa ziara hiyo uliipongeza kampuni hiyo kwa kuwakaribisha pamoja na kuonyesha
ushirikiano mzuri wa kazi kati ya wafanyakazi wa Tanzania na Kichina.
Kusudi kuu la ziara hiyo ni
kuhamasisha maendeleo katika vyombo vya habari kupitia ubunifu, utafiti na
maendeleo ya Sekta ya Vyombo vya Habari nchini Tanzania na China na jinsi ambavyo
wanaweza kushirikiana.
Na: Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment