nEWS: JUVICUF wasema 'it is enough'.. wamechoshwa na 'wasaka tonge'.. 'wampa 5' Mtatiro.. #share

JUMUIYA ya Vijana Chama cha Wananchi (JUVICUF), imesema imechoshwa na vitendo walivyodai kuwa ni vya kipuuzi vinavyofanywa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi na maslahi ya wale wanaowatuma ili kukiua chama hicho. 


Aidha, JUVICUF imepongeza maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa chini ya Mwenekiti wa Kamati ya Uongozi Julius Mtatiro, Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi mbalimbali za kitaifa kwa kuendelea kupigania chama hicho.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Uenezi wa JUVICUF, Abeid Bakar katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana.

Alisema JUVICUF Tanzania na dunia haijawahi kushuhudia hali ya machafuko lakini kwa hali inayoendelea katika chama chaon inatoa viashiria vya kuelekeav huko jambo ambalo wasingependa kuliona.

“Hakuna shaka yoyote kua Rais John Magufuli na dunia haijawahi kushuhudia Tanzania ikichafuka ila hujuma hizi zikiendelea kufanywa wao kama vijana watashindwa kuvumilia,” alisema.

Bakar alisema JUVICUF ipo tayari kukilinda chama na kulinda maslahi ya wanachama wake na Watanzania kwa ujumla kwa gharama yoyote ile.

“Tukumbuke kua wenzetu wengi walishapoteza maisha kwa ajili ya kupigania maslahi ya Watanzania kupitia CUF, hivyo sisi hatutokua wa mwanzo na hatutokua tayari kuisaliti damu ya wale waliopigania maslahi hayo kama haki itazidi kuminywa,” alisema.

Naibu huyo wa JUVICUF alisema wanapenda kuwaarifu wanachama wa CUF na Watanzania kwa ujumla kua sasa inaandaa utaratibu wa kupambana na hujuma za Profesa Ibrahim Lipumba kwa vitendo hivyo.

Alisema JUVICUF haiko tayari kuona kila siku Katibu Mkuu wao na viongozi wake wanasumbuliwa na kikundi cha watu nane kinacholindwa na dola,”inatosha inatosha,”.

Bakar alisema JUVICUF kwa sasa haitokubali tena kuona uhuni huu ukiendelea kufanyika na itachukua hatua madhubuti kwa wale wote wanaoshiriki kutekeleza hujuma dhidi ya chama chao.

Alisema JUVICUF kabla haijachukua hatua ambazo inapanga kuzichukua kwa wale wote wanaosababisha hujma hizi inamtahadharisha Raisi Magufuli juu ya muendelezo wa mihimili yake katika kutekeleza hujuma dhidi ya CUF. 

JUVICUF inafahamu fika kuwa yanayoendelea kutokea kuhusu CUF ni muendelezo wa ushahidi kuwa hujuma dhidi ya chama hicho ni mkakati mahususi wa kukipunguzia nguvu na kukifuta chama hicho ambacho kimekua mwiba mkubwa kwa upande wa Zanzibar na hatari zaidi umoja wake na nguvu inayopatikana katika UKAWA,

“Lakini pia ni chma chenye Wanachama /wafuasi na mtandao wa kiuwakilishi ulioenea pembe zote za nchi nzima Bara na Zanzibar,” alisema.

Aidha, alisema JUVICUF inawapongeza viongozi wote na inaunga mkono maazimio yote ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kuwaomba wanachama wasitetereke na kuendelea kuwa wastahamilivu na kuwaskiliza viongozi wao.

Bakar alisema kinachohitajika ni kila mwanachama kuwa na umakini na uadilifu kwa wale wenye majukumu yakiwemo ya kimkakati.

Alisema JUVICUF pamoja na kuwapongeza viongozi hao pia inaunga mkono maazimio yote yaliyotolewa na Baraza Kuu. 

Naibu mkurugenzi huyo alisema wanaamini kuwa maazimio hayo yameleta matokeo chanya kwa wanachama, wapenzi wa CUF na Watanzania kwa ujumla hasa baada ya wengi wao kufadhaishwa na kile alichokifanya Spika wa Bunge Job Ndugai ambapo bila ya aibu aliamua kubariki uharamu wa Lipumba na genge lake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search