nEWS: Meya UKAWA amwangukia JPM anusuru Mradi wa DMDP jijini Dar es Salaam...#share

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (Chadem) amemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati ucheleweshaji wa kusainiwa kwa fidia ya sh biloni 14 ili kuwezesha upatikanaji wa fedha za Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP).
Pichani ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob
Rai hiyo imetolewa leo na Jacob wakati akifungua mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ubungo na kueleza kuwa mradi wa DMDP jijini Dar es Salaam kutoka Benki ya dunia ni Sh bilioni 600.
Amesema kumekuwepo na hali ya viongozi wa serikali kutaka kukwamisha miradi ya maendeleo katika maeneo ambayo yana viongozi wa upinzani.
Alisema miriadi hiyo ya DMDP ilianza tangu 2013/14 na ilikusudiwa kutekelezwa Kinondoni na Ubungo kabla ya kugawanywa, alieleza kuwa Ubungo kwa sasa ndiyo inaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mkwamo huo.
“Kwa masikitiko makubwa tumewasiliana na Mkuruenzi wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika, wiki mbili hizi wametuambia mkwamo uliopo,” alisema Jacob.
Amesema kuwa fedha hizo sh. bilioni 600, WB wamekaa nazo tangu mwaka 2015/16 na 2016/17 na kubainisha kwamba akiwa Kinondoni waliidhinisha benki iwakopeshe kwa ajili ya ulipaji wa fidia lakini viongozi wa serikali wamekataa kusaini hivyo Ilala, Kinondoni na Ubungo kuzikosa huku fidia ya Temeke pekee zikisainiwa kutoka benki ya CRDB.
Meya Jacob amebainisha kuwa Uongozi wa WB chini ya Mkurugenzi wake Billa Bird wamekuwa wakifanya juhudi ya kuwasiliana na viongozi wa serikali ili kukutana na kujadili jinsi ya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo, lakini wamekuwa hawajibiwi.
Ameweka wazi kwamba mara ya mwisho kwa viongozi wa WB kuomba kukutana na viongozi wa serikali ilikuwa ni Juni 1 mwaka huu ambapo siku hiyo walipofika sehemu ya mkutano walijikuta wakiwa wenyewe pasipo ujumbe wa serikali kufika.
Amesema kutokana na hali hiyo hivi karibuni alifahamishwa kwa barua WB wataondoa fedha hizo katika miradi hiyo na kuhamishia kwingine ikiwa serikali haitachukua hatua za haraka ili kupata mwafaka wa fidia hiyo kwa ajili ya fedha hizo kutolewa tayari miradi kuanza kutekelezwa.
Amebainisha kuwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mkwamo huo wanakosa kiasi cha sh. bilioni 51 ambazo zilkuwa zimeelekezwa katika miradi tisa na miongoni mwa miradi hiyo ni barabara ya mawasiliano (Simu 2000), barabara kuanzia Sinza Kijiweni kupitia kwa Mtogole hadi Morocco na kadhalika.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment