sPORTS nEWS: UEFA yaishushia rungu kali Manchester United, pia yafungia wawili....#share

Chama cha Soka Barani Ulaya (UEFA) leo kimetangaza kumfungia mchezaji mwingine wa klabu ya ‘Mashetani Wekundu’ Manchester United Phil Jones mechi mbili, kwa kosa la kukataa kuchukuliwa vipimo vya utumiaji wa dawa zisizoruhusiwa michezoni na kuendelea kufurahia na wenzake ubingwa wa Europa.


Adhabu hiyo imekuja baada ya siku kadhaa toka beki wa kimataifa wa Ivory Coast anaekipiga na klabu hiyo Eric Baily kufungiwa michezo mitatu na chama hicho.
Aidha adhabu hazikuishia kufungiwa mechi tu bali pia wote wamelimwa faini ya pauni 4500 kwa kosa hilo la kwa makosa hayo ya utovu wa nidhamu kwa waliyotenda kwa maofisa wa UEFA.

Aidha Adhabu ya UEFA haikuishia kwa wachezaji hao bali club pia ya Man United imepigwa faini ya pound 8,900 kwa kuvunja sheria kwa kushindwa kuhakikisha wachezaji wake wanapima.


Pamoja na rungu hilo UEFA imewapa Man United siku tatu za kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Chanzo: Sport360

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search