PICHA 23: JPM amfariji Dr. Mwakyembe,.. aendesha harambee kanisani Chato na kufanikiwa kuchangisha Tshs. milioni 13, ahadi Tsh laki 9 na mifuko 33 ya saruji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Leo July 16, 2017 ametuma Salamu za Rambirambi kwa Waziri wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe aliefiwa na mkewe Bi. Linah George Mwakyembe aliefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 15/07/2017 na kuelezea kuguswa kwake na kifo cha Bi Linah.
Wakati huo huo Rais amehudhuria Ibada ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Katika harambee hiyo Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amefanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 13, ahadi Shilingi 920,000/=, mifuko ya saruji 33 na malori 2 ya mchanga.






No comments:
Post a Comment