SPORT News: Simba yakwea pipa kuitafutia dawa Yanga Afrika Kusini...# share
Timu ya Soka
ya klabu ya Simba kesho alfajiri, inatarajia kwenda nchini Afrika kusini, kwa
ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu, unaotarajiwa kuanza mapema mwezi
ujao.
Kambi hiyo ya siku Ishirini itahusisha wachezaji wote
waliosajiliwa kwenye klabu, kwa msimu huu wa ligi.
Kwa upande wa wachezaji waliopo kwenye Timu ya Taifa, wao
wataungana na wenzao, mara baada ya mchezo wa marudiano baina Taifa Stars na Rwanda,
utakaochezwa wiki ijayo kule Kigali.
Ikiwa huko nchini Afrika kusini, kikosi hicho pia kitapata
fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu, kabla ya mchezo wake wa
tarehe nane mwezi ujao(SIMBA DAY), Mechi ambayo klabu huitumia kutambulisha
wachezaji wake na jezi mpya ya msimu, mchezo huo utapigwa hapa jijini Dar es
salaam,kwenye uwanja wa Taifa.
Wakati huo huo klabu ya Simba inaungana na wanamichezo na
watanzania wengine, kumpa pole Waziri wetu mwenye dhamana ya michezo nchini Dr
Harrison Mwakyembe kwa kuondokewa na Mkewe bi Linnah Mwakyembe.
Tunamuomba Waziri Mwakyembe awe na subira yeye na familia
yake katika kipindi hiki kigumu,na klabu itashiriki shughuli zote za msiba wa
mama yetu Linnah
*IMETOLEWA NA*
IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO
SIMBA SPORTS CLUB
No comments:
Post a Comment