Tetesi za usajili: Mbappe afanya kufuru; 'kulala mbele na mkataba wa miaka 6 Madrid'.. Zidane amhakikishia namba.. #share

Klabu ya Real Madrid imekubali kulipa kitita cha £160m kwa ajili ya kukamilisha dili la Mshambiliaji wa Monaco ya Ufaransa Kylian Mbappe (18).


Kwa mujibu wa Daily Mail online ni kwamba mchezaji huyo atasajiliwa kwa mkataba wa miaka sita.

Endapo dili hilo litakamilika litavunja rekodi ya usajili wa Paul Pogba mwaka jana aliposajiliwa kutoka klabu ya Juventus kwenda Manchester United kwa ada ya pauni milioni 80
Rais wa klabu hiyo Florentino Perez alijaribu kumsajili mchezaji huyo mapema katika majira haya ya joto lakini familia ya Mbappe na washauri wake walikataa kwa kusema kuwa si mahali sahihi kwake.
Aidha Kulikuwa na hisia kuwa angeweza kupata shida katika kupata muda wa kucheza kwenye klabu hiyo ya Real Madrid kutokana na klabu hiyo kuwa na magwiji wa soka wengi.

Lakini baada ya mchezaji huyo kufanya mazungumzo na Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemhakikishia namba katika kikosi hicho .

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search