Top News.. Makene 'aanika vikwazo viwili anavyopambana navyo Lissu leo..' #share.. 'Wanasheria bado wahoji kipimo cha mkojo..
Afisa habari wa CHADEMA Makao Makuu Tumaini Makene ameelezea uwezekano wa ratiba ngumu leo ya tarehe 24/07/2014 akitaja jumla ya mashauri mawili yanayomkabili Lissu...
Katika waraka alioutuma kwa baadhi ya vyombo vya habari na Matukio360 kunasa nakala yake,.. Makene aliyataja mashauri hayo likiwemo la Mawakili kufungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka polisi wampeleke mteja wao Mahakamani haraka..
"..Shauri la pili linatarajiwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako polisi, kwa mujibu wa sheria, wanatarajiwa kumfikisha mahamakani Lissu baada ya kumshikilia na kumweka mahabusu zaidi ya masaa 24. It is tricky, lakini ndivyo hali yenyewe ilivyo...." alimaliza Makene akielezea shauri la pili na kuwahimiza waandishi kufika maeneo ya tukio mapema akisisitiza kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa Lissu kufikishwa Mahakamani leo..
====================
Wakati huo huo Wanasheria nchini wamehoji sababu za Lissu kuchukuliwa kipimo cha mkojo wakati akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi.
Kwa mujibu wa wanasheria hao, makosa yanayoweza kusababisha mtuhumiwa achukuliwe kipimo hicho ni ya usalama barabarani, matumizi ya dawa za kulevya, ubakaji na mashauri ya ndoa na watoto ambayo hulazimu mkemia kupima sampuli hizo.
“Mtuhumiwa anaweza kukataa kupimwa mkojo kwa amri. Polisi nao hawaruhusiwi kutumia nguvu. Wanachoweza kufanya ni kutafuta amri ya mahakama ili kumlazimisha mtuhumiwa kukubali kupima au akabiliane na kifungo kwa kukaidi amri ya mahakama.” Alieleza Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk James Jesse aliyeulizwa kuhusu tuhuma zinazoweza kusababisha kuchukuliwa kwa kipimo hicho, huku Mwanasheria mwingine, Benedict Isahabakaki alisema kitaalamu, polisi walitakiwa kumweleza mtuhumiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili na kifungu cha sheria ambacho wanadhani amekivunja.
“Vipimo vya mkojo havina uhusiano wowote na makosa ya uchochezi. Tatizo ni kwamba polisi wamekuwa wakifanya kazi zao kienyeji, ndiyo maana wanawakamata watuhumiwa wengi Ijumaa wakidhani kwamba hawawezi kutoa dhamana siku za wikiendi, kitu ambacho ni makosa. Polisi wanatakiwa kufanya kazi hata wikendi,” alisema mwanasheria huyo.
Lakini Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema uchunguzi wa polisi hauna mipaka na kwamba jeshi hilo halifanyi kazi kwa mihemko ya watu, bali kwa kuzingatia weledi.
“Kwenye suala la ku-suspect (kutuhumu), polisi anaweza ku-suspect anything (kitu chochote) kutoka kwa mtu yeyote. Siwezi kuelezea mikakati na mbinu za kiuchunguzi, lakini mtambue kwamba uchunguzi is too general (ni mpana), unaweza kuchunguzwa kwa mambo mengi,” alisema Mwakalukwa...

No comments:
Post a Comment