News: JPM aamua 'kulala mbele' na 'mafataki'.. share.. aonya Bilioni 19 kwa mwezi sio za 'kimchezo mchezo..'

Rais Magufuli amesema siku hizi siyo vijana peke yao wanao haribu wanafunzi, na kwamba wapo wazee walioko shapu na hawapitwi kuwapa mimba wanafunzi, na kuwataka wenye tabia hiyo waache kwa sababu watafungwa kwa miaka 30. 




Rais John Magufuli amesema wanaowapa mimba wanafunzi hawana budi kufungwa miaka 30 ili kukomesha suala hilo na kuwapa fursa watoto wasome kwani hao ndiyo viongozi wa kesho.

Rais amezungumza hayo jana wakati wa uzinduzi wa barabara Kaliua, mjini Tabora, ambapo aliweka wazi kwamba wanaowapa mimba watoto wa shule siyo vijana pekee bali wapo wazee nao wameingia kwenye mkumbo huo hali ambayo inawafanya mabinti washindwe klumaliza elimu ya sekondari.

“Wazee siku hizi wapo shapu kuliko vijana, wanawapa mimba wanafunzi, muwaache wasome, ukimpa mimba mwanafunzi unafungwa miaka 30 nguvu zako zikaishie gerezani,” amesema na kuwataka wanafunzi kusoma ili watimize ndoto zao. Soma kwanza, usipate mimba ukiwa shule, subiri umalize sekondari ndipo upate mimba,” amesema.

Pamoja na hayo Mhe. Magufuli amesema kuwa serikali yake imedhamiria kuwapatia wanafunzi wa kitanzania elimu.

"Tumeamua kutoa elimu ndiyo maana tumetenga bilioni 18.777 tunataka watoto wasome na wasipate mimba, naomba wajiepushe na mimba mpaka watakapotimiza malengo yao," aliongeza - EATV

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search