Trending News!! CUF Watimua Wabunge wanane Viti Maalum.. #share

Chama Cha Wananchi CUF kimewavua uanachama wabunge 8 wa viti maalum na madiwani 2 kwa madai ya kushirikiana na CHADEMA kufanya usaliti ndani ya chama..



Taarifa ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF - Kambi ya Prof. Lipumba, limetangaza maamuzi hayo mchana huu na kubainisha fyagio maalum la kusaka wasaliti na kukisafisha chama linaendelea.. 

Hapo jana Wabunge 10 na madiwani wawili wa CUF, waliiitwa mbele ya kamati ya nidhamu kwa ajili ya mahojiano katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni, ingawa hadi kufikia majira saa 5.00 asubuhi hakukuwa na aliefika miongoni mwa walioitwa.. 

Wabunge hao wanaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad waliitwa ili kuhojiwa na kamati hiyo kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya CUF.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search