bREAKING nEWS: Haya Hapa Mashtaka aliyosomewa Lissu.. mwenyewe akana,.. hoja ya dhamana inaendelea kujadiliwa.. #share
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu, amepandishwa kizimbani mchana huu na kusomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika maeneo ya Ufipa, Kinondoni.. mnamo siku ya Julai 17, 2017
Katika hati ya Mashtaka, inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya viongozi ndani ya Jamuhuri ya Tanzania.
Lissu amepandishwa mahakamani hapo , mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri, na amekana shtaka hilo..
Hata hivyo, upande wa mashtaka wameomba mahakama anyimwe dhamana huku upande wa utetezi wakipinga hoja hiyo.
Kumekuwepo na mvutano mkali juu ya dhamana ya Lissu, ambapo Mahakama imeamuru arudishwe rumande hadi siku ya Tarehe 27 atakaporudishwa tena Mahakamani..
No comments:
Post a Comment