tRENDING nEWS: Masaa machache baada ya kutoka rumande, Tundu Lissu aitisha press na kunena mazito.. #share

MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maeneleo (Chadema) amesema ataenedelea kuzungumza na kumkosoa rais kwa kuwa ni haki yake kikatiba.


Kauli hiyo amaitoa leo jijini Dar es Salaam akizungumza na wanahabari baada ya kuachiwa kwa dhamana, amesema hatokaa kimya huku akibainisha kwamba kitakacho mzuia ni kifo pekee.

Amesema hatua ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu na hata kufungwa, hakutomzuia yeye kusema ama kumkosoa Rais kwani akiwekwa mahabusu au kufungwa atazungumzia akiwa kifungoni.

"Wanataka tunyamaze ili waendeshe nchi hii wanavyotaka wao, Taifa hili ni la mfumo wa vyama vingi tunayo haki ya kufanya mikutano, tunayo haki ya kufanya maandamano na tunayo haki ya kutoa maoni yetu.Kwa msingi huo hakuna wa kutunyamazisha nchi hii siyo mali ya mtu binafsi"

"Ukisema unakumbana na segerea, ili tumuachie yeye peke yake, hatutamuachia yeye peke yake, hakuna gereza litakalotunyamazisha.. sio atupeleke mahabusu sababu tutazungumza tukiwa huko, hata akitufunga tutasemea tukiwa kifungoni"

"Njia rahisi ya kwenda mbinguni ni kupinga uonevu, itabidi tufe kwanza ili tusiseme, mwambieni Magufuli tutanyamaza tukiwa wafu kwasababu wafu huwa hawasemi".

Lissu amesema kua kitendo cha kunyamaza kinaweza kusababisha nchi ikaangamia, na kuongeza kuwa hakuna atakayeweza kuwanyamazisha.

"Hakuna wakutunyamazisha, kwasababu tukinyamaza kwa kuogopa mahabusu tukaogopa mabomu ya polisi, tukanyamaza nchi hii inaangamia".

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search