UTAFITI: Mradi wa Masava (Mafuta Asili ya Alizeti yenye Vitamini A) kutatutua tatizo la utapiamlo kwa kina mama wajawazito na watoto nchini..#share
UTAPIAMLO umetajwa kama moja ya matatizo sugu ya kiafya
nchini yanayoathiri makundi yaliyohatarini kama vile watoto wachanga, watoto
wadogo na wanawake waliofikisha umri wa kushika ujauzito.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mtaamu wa Lishe na Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Profesa Theobald Mosha katika mkutano wa kufunga Mradi wa Masava (Mafuta Asili ya Alizeti ya Vitammini A).
“Utapiamlo ni changamoto kubwa ya maendeleo nchin Tanzania,
walakini mradi uliohusisha wadau mbalimbali umesaidia kulishughulikia suala
hili kwa kuyafanya mafuta ya kupikia yenye vitamin A yapatikane kwa wingi ili
kukabiliana na tatizo hilo,” alisema Profesa Moshi.
Amesema katika maeneo mengi ya vijijini milo inakosa virutubisho
vya msingi kwa ajili ya kujenga kinga thabiti ya mwili ili kuwa na afya bora na
kupambana na magonjwa hususani kwa wanawake na watoto.
Profesa Mosha amebainisha kuwa katika muongo uliopita watoto
wanaokadiriwa kufikia 600,000 walio chini ya miaka mitano walifariki nchini
kutokana na upungufu wa virutubisho vya lishe.
Ameeleza kwamba
changamoto kubwa ni upungufu wa vitamin A ambapo alisema ni kwa robo tatu ya
watoto walio chini ya miaka mitano na asilimia 37 ya wanawake wanye uumri wa
miaka 15 hadi 49 wanaosumbuliwa na tatizo la upungufu wa vitamin A.
Mradi huo wa miaka mitatu uliokuwa chini ya shirika la
Mennonite Economic Development Associates (MEDA), Chuo Kikuu cha Waterloo na
Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) wamethibitisha tatizo la upungufu wa virutubisho
vya vitamin A linaweza kutatuliwa kwa kutumia kwa kutumia mafuta yaliyoongezwa
virutubisho ambayo ndiyo hayo maalumu ya MASAVA.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dk. Ulisubisya Mpoki amesema mradi huo upo katika ajenda kubwa
ya lishe nchini ambapo alieleza serikali inaendelea kuweka msisitizo juu ya
suala hilo.
Aidha amesema licha ya kupiga hatua katika kuliboresha suala
hilo bado mamilioni ya wanawake na watoto wanaendelea kuteseka na aina
mbalimbali za lishe duni. Alisema mradi wa mafuta hayo yenye vitamin A
unaendana na ajenda ya kitaifa ya kulichunguza tatizo hilo sugu kwa jicho la
kiubunifu na kwa wigo mpana.
Alisema serikali imeweka nia kikamilifu kwa ajili ya fumbuzi
za kibunifu za suala la utapia mlo na usalama wa chakula iliyosisitizwa kupitia
mpango wa scaling up Nutrition.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment