ONYO: Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani halitakuwa na msamaha kwa madereva wavunjifu wa sheria kwa mwanvuli wakutopewa elimu..#share
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini limesema
halitasita kutoa adhabu kwa madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani
kwa kisingizio kuwa hawana elimu juu ya makosa hayo na pia kutoelezwa sababu za
kukamatwa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa
Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Fortunatus
Musilimu, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano
ulioitishwa na wizara ya mambo ya ndani uliokuwa na lengo la kuuarifu umma
kuwepo kwa tamasha kubwa Agosti 5 mwaka huu lilioandaliwa na Baraza la Usalama
Barabarani Taifa.
Aidha ameeleza kuwa taratibu na sheria za jeshi hilo
zinamtaka polisi anapomkamata mtu kumwelezak sababu za kumkamata kwa kutaja
kosa lake.
“Lazima ajulishwe tatizo lake, ndiyo sehria inavyosema,
lakini nachotaka kusema na niwe muwazi kabisa kuna baadhi ya madereva ambao
makosa ya usalama barabarani wanayachukulia kama ni makosa madogo madogo ya
kuchezea chezea wanafanya mzaha, mzaha ambao unapelekea kutokea kwa ajali
ambazo ndizo zinasababisha vifo vya watu,”
“Wewe ni dereva umepata mafunzo ya udereva unategemea tukupe
elimu gani barabarani, unategemea tukupe elimu gani barabarani?, sasa nasema
hivi kwa dereva anayetegemea akamatwe amefanya kosa tumpe elimu barabarani hilo
hatutafanya kama unetegemea kupata hiyo elimu barabarani ni afadhali usiingize
gari lako barabarani kwani hatutafanya hivyo na tutakuchukulia hatua pale pale,”
alisema Kamishna Musilimu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani Taifa akizungumzia tamasha hilo
lililoandaliwa, amesema ni mkakati wa awamu ya pili katika kupunguza ajali za
barabarani.
Amesema lengo la tamasha hilo
ni kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa usafiri ili kupunguza au kuondoa
tatizo la la ajali. Alitaja wadau hao kuwa
ni pamoja na watumiaji wa usafiri, wamiliki wa vyombo vya usafiri,
madereva na wananchi.
Aidha amesema kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo anatarajiwa
kuwa Rais John Magufuli.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment