GUMZO: Basi unaambiwa hayo madeni ya Sahara Media 'usipime..'

KUYAHUSU MADENI SAHARA MEDIA: Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sahara Media Group (SMG), inayomiliki kituo cha televisheni Star TV, Redio Free Africa (RFA) na Kiss FM anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara.



Mkurugenzi huyo atafikishwa katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kwa kushindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake 20 kiasi cha zaidi ya Sh milioni 100 ikiwa ni malimbikizo ya kipindi cha miezi 16 sawa na mwaka mmoja na nusu.

Mahakama hiyo inatarajiwa kusikiliza mashauri 15 yote yakiwa ya madai ya malimbikizo ya mishahara ambayo yatasikilizwa Julai 21, mwaka huu, ambayo tayari Tume ya Utumishi na Usuluhishi imeagiza wafanyakazi hao walipwe.

Julai 13 mwaka huu, kampuni hiyo, ilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushindwa kulipa kodi ya Sh. 4.5 bilioni ambapo tayari wiki moja imekatika na taarifa zinadai hajalipa hata senti moja.

Katika hatua hiyo kampuni ilipewa siku 14 (wiki mbili) kuanzia Julai 13 mwaka huu, iwe imelipa kiasi hicho cha fedha na kama haitafanya hivyo majengo ya kampuni hiyo yanaweza kupigwa mnada ili kufidia deni hilo ambalo ni malimbikizo ya kodi ya kipindi cha awali huku kipindi cha miaka miwili 2016/17.

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo (jina linahifadhiwa) aliueleza kuwa wamelazimika kwenda Mahakamani baada ya Kampuni kushindwa kutekeleza makubaliano yao, yaliotolewa na Tume ya Utumishi na Usuluhishi (CMA).

Alieleza kwamba wanataka kuiomba mahakama kuagiza mara moja walipwe fedha zao mara moja au la Mahakama iangize wauze asset ili walipwe stahiki zao.

"Mwajiri wetu amekuwa akitoa ahadi bila kutekeleza, ndiyo maana hata kampuni yake ilifungiwa na TRA baada ya kupewa mwaka mmoja awe amelipa madeni yake lakini alishindwa na akafungiwa,” amesema mfanyakazi huyo.

Pia amedai kumekuwa na udanganyifu mkubwa unaofanywa na mwajiri kwa kutokupeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii PPF/NSSF na hata inayopelekwa imekuwa na taarifa za uongo ambayo michango inayowasilishwa hailingani na mishahara ya wafanyakazi.

Taarifa nyingine kutoka ndani ya kampuni hiyo zinaeleza kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeipunguzia masharti kampuni ya Sahara ya kulipa deni lake kwa awamu kwa kuanza na Bil. 2 badala ya kulipa deni la Sh. 4.5 bilioni kwa mkupuo.. jambo ambalo pia limeshindikana..

Kwa upande wake, Mgurugenzi huyo amekiri kuwepo na wafanyakazi wanaomdai lakini alidai hawazidi wawili huku akishindwa kuweka wazi kiasi wanachomdai.









About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search