BREAKING: JPM 'atibua' Kata 25 uchaguzi CCM.. Polepole ataja 'dawa' kwa waliboronga.. asema wengine walidiriki kujipangia 'safu za Viongozi wao'.. #share
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimesema kitawaita kwenye Kamati
ya Madili na kuwahoji wagombea waliovuruga uchaguzi wa ndani kwenye maeneo
mbalimbali katika uchaguzi wa ndani unaoendelea nchini na kuwachukulia hatua
kwa mujibu wa Katiba yao.
Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea changamoto zilizojitokeza katika chaguzi hizo.
“Watu hawa wanaoendeleza makundi
ndani ya chama chetu ni wasaliti, tunataka viongozi ambao watakitumikia chama
na wananchi kwa uadilifu mkubwa, na hii ndiyo dhana ya CCM Mpya,” alisema
Polepole.
Alitaja changamoto ambazo
zimejitokeza katika uchaguzi huo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa makundi ambayo
yamekuwa yakipanga safu za viongozi wanaowataka lakini pia baadhi ya maeneo
kutowatendea haki wanachama katika upitishwaji wa wagombea.
Polepole alisema kutokana na
changamoto hizo Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli na Katibu Mkuu wake
walipokea malalamiko na kero za uchaguzi huo kutoka kwa wanachama. Baada ya
kuzipokea Mwenyekiti alimwagiza Katibu kufuta chaguzi katika maeneo yaliyokuwa
na dosari hizo.
Alitaja kata 24 ambazo chaguzi hizo
zimefutwa na kuwa zitarudiwa kwa kutolewa
fomu upya kwa wanachama na kurejeshwa.
Maeneo ni kata za Lumemo-Kilombero,
Seriya kwa Vijana-Kondoa, Kariakoo, Liwiti, Manzese, Buguruni, Mianzini,
Makuburi, Kigamboni, Gerezani, Segerea, Pugu Stesheni, Pugu, Kitunda, Ukonga,
Msasani, Makumbusho, Mabibo na Ndugumbi zote za Dar es Salaam.
Nyingine ni kata za Mapinga-
Bagamoyo, kata zote za Simanjiro mkoani Manyara na Mchafukoge.
Na Abraham Ntambara



No comments:
Post a Comment