KIMENUKA: TLS yawataka wanachama wake kususia Mahakama kwa Siku Mbili.. Kisa!? kuomboleza kulipuliwa Ofisi ya Fatma Karume.. #share
BARAZA la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS),
limewataka wanachama wote wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria katika Mahakama
pamoja na Mabaraza ya aina zote kesho kutwa na Jumatano Agosti 29 hadi 30 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Rais wa TLS Tundulisu lengo likiwa ni kuunga mkono mawakili wa IMMMA Advocates na kuonyesha kutokubaliana kwao na vitendo vya kihalifu vya kuwashambulia mawakili hao kwa mabomu.
Itakumbukwa kuwa usiku wa kuamkia jana Ofisi za IMMMA
Advocates zinazomilikiwa na wakili Fatma Karume na Lawrence Masha zilizoko
jijini Dar es Salaam ziliungua moto kutokana na shambulio la mabomu.
“Kitendo cha kushambulia Ofisi za IMMMA Advocates kwa mabomu
na kusababisha uhalifu wa ofisi hizo ni kitendo cha kigaidi kwa mujibu wa
kifungu cha 4(3) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi, 2002,” amesema Lissu.
Amebainisha kuwa kitendo cha kushambulia ofisi hizo kwa
mabomu kina lengo la kuwatisha mawakili hao wasiweze kutekeleza wajibu wao kama
wanasheria na mawakili kwa kuwatia hofu ya kuwadhuru kimwili au kuwapotezea
maisha.
Amesema licha ya kuwataka mawakili kutokwenda kazini katika
siku hizo, Baraza hilo limevitaka vyama vya ulinzi na usalama kutumia mamlaka
vilivyonavyo ya kuipelelezi kuhakikisha kwamba smabulio hilo linachunguzwa kwa
kina ili kuwezesha kujulikana kwa wahusika na kuchukuliwa hatua zinazostahili
kisheria dhidi yao.
Lissu ameeleza pia Baraza limevitaka vyombo vya ulinzi na
usalama kuwahakikishia ulinzi na usalama wa kutosha mawakili wa IMMMA Advocates
dhidi ya vitisho au vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama wao wa
kitaaluma.
Ameongeza kuwa watafanya jitihada za haraka kukutana na
Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa
(TISS) pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ili kujadiliana juu ya shambulio
hilo na usalama wa mawakili wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kitaaluma.
Aidha amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama, uhuru
na heshima ya wanasheria na kuwawezesha mawakili nchini kutekeleza wajibu wao
wa kitaaluma wa kulinda utawala wa Sheria na Haki za Binadamu.
Na Abraham Ntambara



No comments:
Post a Comment