Breaking: 'Mkojo wa Manji' wazua utata Mahakamani.. Mkemia asema hajui kama ni wa Manji au wa Polisi aliemsindikiza chooni.. #share

Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic ameieleza Mahakama ya Kisutu leo August 23, 2017 kuwa dawa za kulevya (Benzodiazepines) alizobainika anatumia mfanyabiashara Yusuf Manji zinatolewa hospitalini na zinauzwa Pharmacy.



Mkemia huyo amesema hajui kama sampuli ya mkojo alioupima ni wa Manji ama Askari Polisi, kwa sababu wakati Manji anachukuliwa sampuli hiyo aliingia chooni na Askari, huku yeye akiwasubiri nje.Wakili huyo alihoji jambo hilo ili mashahidi waithibitishie mahakama kwani wakati Manji anakwenda msalani kutoa sampuli hiyo ya mkojo aliongozana na askari, jambo ambalo lilifanya wasikilizaji wa kesi hiyo waangue vicheko ndani ya mahakama.

Aidha, Mkemia amesema katika kipimo cha mkojo wa Manji amebaini uwepo wa dawa aina ya Benzodiazipines ikiwa ni zao la Heroin, ambapo dawa hiyo ina matumizi mengi ikiwemo kuondoa maumivu makali, ikitegemeana na ushauri wa daktari.

Baada ya kuelezwa hayo, Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis amesema Serikali imefunga ushahidi wa mashahidi wake watatu. Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema atatoa uamuzi kama Manji ana kesi ya kujibu ama la, August 25/2017.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search