Breaking: Polisi Dar wafanya upekuzi nyumbani kwa Tundu Lissu.. #share

Polisi jijini Dar es Salaam, leo hii tarehe 23/08/2017 wamefanya upekuzi nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Mbunge MHE. Tundu Lissu.
Taarifa iliyotolewa na mchana huu imesema kwamba Jeshi la Polisi Dar es salaam limemaliza upekuzi nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu.
Baada ya kumaliza upekuzi huo limemrudisha Lissu tena kwenye kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria kuendelea, ikiwa ni pamoja na dhamana yake ambayo alinyimwa hapo jana.
Hii ni mara ya pili Polisi wanapekua nyumba ya Lissu ambapo mara ya mwisho mnamo Julai 21, Polisi walipekua na kuondoka na CD sita za Lissu zilizohusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na mgodi wa Bulyanhulu mwaka 1999.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search