Breaking News: TEF, Makonda, Ruge.. 'kamatia chini'.. Makonda agoma kuomba radhi.. TEF, Boss Ruge wakubali yaishe.. #share..

MKUTANO uliokuwa ukiendea mida hii ndani ya Holiday Inn umemalizika 'kibingwa' huku pande tatu zilizokuwa kwenye sintofahamu 'zikikubali yaishe' na kuondoa rasmi zuio la TEF la kuzuia vyombo vya habari kuripoti taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam RC Makonda licha ya kukataa kuomba radhi kwa tukio la uvamizi wa kituo binafsi cha Television cha Clouds kilichopo Mikocheni.



Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo cha Cloudz Bw. Ruge Mutahaba, amesema amekubali yaishe, kwa heshima ya Rais MHE JPM, lakini nafsi yake ni nzito juu ya suala zima ambalo anaamini kwa asilimia 100% kuwa RC Makonda amehusika nalo.. 
Akijitetea juu ya msimamo wake wa kukataa kuomba radhi, Mhe. RC Makonda amesema askari aliokuwa nao ni kwa ajili ya usalama wake, na kumchunguza kimaadili kama mtumishi wa Umma; huku akikataa katakata kuwa alivamia kituo hicho... 
RC Makonda ameilaumu TEF kwa kutoa maamuzi ya upande mmoja..
Kaa na matukio360 tukiendelea kukupasha yanayojiri katika sakata hili ambalo nyota ya matumaini imeanza kuonekana... 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search