Odinga apinga Matokeo ayaita ya Computer,.. adai anaongoza kwa kura 8.7million vs 7.4million za mpinzani wake..!!
Mgombea urais wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga amepinga matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo, IEBC

Bw Odinga amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu ufaao.
Bw Odinga amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu ufaao.
Waziri mkuu huyo wa zamani amesema kabla ya matokeo yoyote kutangazwa, IEBC inafaa kuwapa maajenti wa vyama Fomu 34A kutoka vituoni.
Amesema kwa sasa, bila kuwepo kwa fomu hizo, ni vigumu kubaini matokeo yanayopeperushwa yanatoka wapi.
"Mfumo umeacha kufanya kazi. Sasa ni mitambo inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu 34A pekee zinazoonesha chanzo cha matokeo," amesema.
"Kwa hivyo, tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa kwa sasa na kuitaka tume ya IEBC itoe fomu 34A za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa."
IEBC imekuwa ikitangaza matokeo ya urais mtandaoni, na kufikia saa tisa na robo alfajiri, matokeo hayo yalikuwa yanamuonyesha Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee akiwa mbele na kura 6331140 (55.27%) naye Bw Odinga akiwa na kura 5031737 (43.92%).
Matokeo hayo ni ya kutoka vituo 295319 kati ya vituo 40883 nchini humo ambayo Raila ameyaita ya Computer...
Hata hivyo kwa mujibu wa Bw. Mudavadi ambaye ndie wakala Mkuu wa Mgombea Raila Odinga ameyaita matokeo ya IEBC kuwa ya kitapeli huku akionyesha takwimu zinazomuonyesha mgombea wake akiwa mbele ya Uhuru Kenyatta kwa tofauti kubwa ya kura Bw. Odinga akesemekana kuongoza kwa zaidi ya 53% akiyataja matokeo hayo kuwa ni halisi kutoka vituo vya kuhesabia kura.
Real results from polling station constituency level/Nasa polling station Results From NASA Tallying centre.
NASA 53.23%
JP 45.60%
Total Cast Votes: 16,343,850
JP: 7,452,944
NASA: 8,700,539
Others: 190,367
Others : 1.16%
Alitoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kupuuzilia mbali matokeo yanayotangazwa.
No comments:
Post a Comment