Breaking: Spika Ndugai Leo kamalizana na Maalim Seif.. ni hivyo yaani!! #share
Itakumbukwa miezi kadhaa iliyopita Maalim Seif akizungumza na waandishi Wa Habari alimtaja Spika wa Bunge Ndugai kama mmoja wa maadui wanaoendeleza mgogoro wa CUF, alitaja wengine kuwa ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, Ofisa ya Usajili ya Vizazi na Vivo (RITA) na kadhalika.
Kauli hiyo Ndugai ameitoa jioni hii wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari alipotakiwa kitoa kauli kwa kutajwa na Maalim kama mmoja wa maadau wa Chama cha CUF, amesema tangu Machi mwaka huu alipokea taarifa ya Msajili kuwa kiongozi huyo anamuda hajafika ofisini.
"Mimi watanzania wrote ni ndugu zangu na sichukii Chama chochote, na kunapotokea suala la utaratibu ni kufuata utaratibu tu,"
"Mwezi Machi mwaka huu nilipokea taarifa kutoka kwa Msajili kwamba Kuna taarifa Maalim ana muda hayupo ofisini na majukumu yote yatakuwa chini ya Naibu wake," amesema Ndugai.
Aidha amefafanua kuwa huo ndiyo msimamo uliopo na kwamba hats akiletewa taarifa kutoka kwa Kiongozi Hugo Wa CUF hawezi ifanyia kazi hadi apate taarifa kama amekwisharudi ofisini.
" sasa kama ni wewe umeletewa taarifa kama hiyo na Msajili ungefanyaje, maana masuala yote ya Vyama hata kunapotokea sintofahamu ndani ya vyama nachofanya ni kupata taarifa kutoka kwa Msajili," amesisitiza.
Amewashauri CUF kusafisha nyumba yao wenyewe na kuacha kkulaumu watu wengine na kusisitiza kwa kuwa Ofisi ya Msajili haimtambui na yeye hawezi kumtambua, anayetambuliwa kwa sasa aliyechua majukumu take ni Sakaya



No comments:
Post a Comment