Breaking: Tundu Lissu atoka rumande jioni hii baada kukamilisha masharti ya dhamana.. #share
Akizungumza mara baada yakutoka nje ya kituo kikuu cha polisi wakili wake Peter Kibatala amesema Lisu ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kurudi tena tare 28 siku ya jumatatu.
Baada ya kutoka nje ya kituo cha polisi Lisu hakutakiwa kuzungumza chochote kutokana na masharti ya dhamana badala yake aliingia moja kwa moja kwenye gari ya wakili wake.
Kibatara amesema Lisu anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi pamoja na kumkashfu Rais.
Lisu alikamatwa Jumanne wakati akitoka Mahakama ya hakimu mkazi kisutu alipowenda kwaajili ya kesi pamoja na kumtetea mteja wake.



No comments:
Post a Comment