bURUDANI: Baada ya Madam Wema, Walper nae kaamua kuja na App yake kwenye Simu za Android.. #share


 Msanii wa Filamu Bongo Jacqueline Wolper ameeleza sababu za yeye kuamua kuja na App.

Wolper atakuwa msanii wa pili kutoka katika tasnia ya filamu kufanya hivyo baada ya Wema Sepetu. Wolper amesema moja ya sababu ni kuwa karibu na mashabiki zake na kuwaepusha kupata taarifa za uongo kuhusu yeye.

“Yeah ni kweli nataka kuja na App yangu na sababu kubwa ambayo imenifanya niwe na App ni kwa sababu mashabiki wengi wanatamanigi kujua vitu vyetu kwa undani kwa sababu wanakutana na facebook fake, wanakutana na mastori fake kwa hiyo ukiwa na App ni kitu kikubwa zaidi kuwaweka mashabiki zako karibu,” alisema Wolper.

Pia ameongeza kuwa“Kuchart nao kuwajibu maswali yao na chochote ambacho wanakisikia wewe unawanyooshea maelezo”.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search