Chadema yatangaza Mgogoro dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Irando....#share

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza mgogoro na mkuu wa wilaya ya Momba mkoni Songwe, Juma Irando kwa kuagiza jeshi la polisi wilayani humo kumuweka ndani kwa saa 48 mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka kwa madai ya uchochezi.


Mgogoro huo umetangazwa leo na Mwenyekiti wa chama hicho katika Halmashauri ya mji wa Tunduma Ali Mwafongo akizungumza na waandishi wa habari,  ameleezea kusikitishwa na amri hiyo ya mkuu wa wilaya na kusema kuwa kamwe hawatarudi nyuma huku akiahidi kutompa ushirikiano mkuu wa wilaya huyo.

“Viongozi wetu wamekuwa wakipelekeshwa sana lakini katu hatutokata tamaa kwa sababu ni kazi yetu kusema ukweli na kuwatumikia wananchi wetu,"

"Uchungu tunaopata tunajua ipo siku itakuwa furaha kwetu kwani ushindi unakaribia. Kinachofanywa sasa hivi wakumbuke ipo siku watawala watakuwa wapinzani na haya yanayofanywa hayataweza kuturudisha sisi nyuma,” amesema Mwafongo.

Aidha mbali na agizo hilo  mkuu huyo wa wilaya pia ametuhumiwa kutoa amri ya kushusha bendera za Chadema hali ambayo imeonesha kuwakera viongozi wa chama hicho.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Irando amekiri kutoa amri ya kukamatwa kwa mbunge huyo kwa madai kuwa ametoa kauli ya kudharau mamlaka ya uteuzi.


Mbunge Mwakajoka amekamatwa jana Jumanne na kuwekwa ndani ikiwa ni siku moja tu baada ya Mbunge mwingine wa Jimbo la Vwawa, Paschal Haonga kukamatwa na jeshi la polisi.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search