Mwigulu Nchemba atoa rai Jumuiya kuwaita na kuwahoji wanaoichafua Tanzania kufukuza wakimbizi wa Burundi...#share
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ametoa rai
kwa wadau wa Jumuiya zinazoshughulikia wakimbizi kama Shirika la Kuhudumia
Wakimbizi Dunia (UNHCR) kuita na kuwahoji watu watakaoendelea kusambaza taarifa
za uzushi kuwa Tanzania inafukuza wakimbizi wa Burundi nchini ili kudhizibitisha.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Nchemba
akifungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Wakimbizi wenye lengo la kujadili na
kuweka mipango mizuri ya jinsi ya kuwarudisha Burundi wakimbizi waliojiorodhesha
kwa hiari yao kurudi nchini kwao.
Amesema kumekuwepo na baadhi ya vyombo vya kimataifa ambavyo
vimekuwa vikidhani kuwa Tanzania inataka kuwaondoa wakimbizi hao kwa nguvu ya
majeshi suala ambalo siyo sahihi.
Amefafanua kwamba sababu ya kusemwa hayo inatokana na vurugu
zilizoanzishwa na wakimbizi wenyewe katika kambi wakishinikiza Jumuiya za
Wakimbizi kuharakisha mchakato wao wakurudi nchini Burundi kwa ajili ya kuwahi
msimu wa kilimo.
Amesema vurugu hizo zilipelekea uharibifu wa mali za wananchi
wa jirani na kambi hivyo ikabidi polisi kuingilia kati kuwatuliza ndiyo
ikachukuliwa kama Tanzania wanataka kuwaondoa kwa nguvu.
“Nimeona hili niliweke sawa kabisaa maana kuna baadhi ya
vyombo vya nje walizani Serikali inafukuza wakimbizi, kwanzia sasa
atakeyeendelea kutoa taarifa hizo ili kuichafua Tanzania, niombe jumuia ya
wadau wa wakimbizi iwaite mizani waeleze wanavyofukuzwa,” amesema Nchemba.
Aidha amebainisha kuwa hali hiyo ya vurugu ilitokea baada ya Agosti 22 Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kukutana na Rais John Magufuli na
kumhakikishia kuwa kwa sasa hali ya Burundi iko shwari na kwamba wanaweka
mipango sawa ili kuwapokea wakimbizi ambao wako tayari kurudi nyumbani kujenga
nchi yao.
Waziri Nchemha amesma hadi sasa
zaidi ya wakimbizi 12,000 wamekwisha jiorodhesha kutaka kurudi nchini Burundi
ambapo waataanza kurudishwa Septemba 7 mwaka huu na kutakuwa na mwendelezo hadi
wote waliotayari kurudi watakapokwisha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa
Burundi Pascal Barandagiye, amesema wakotayari kuwapokea wananchi wao. Na amewahakikishia
kuwa hali iko shwari na kuwataka waendelee kujiandikisha kwa wingi.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment