Bondi Floyd Mayweather akiwa na mkanda wa ubingwa baada ya kumtwanga Conor McGregor kwa Ko, katika pambano lililofanyika leo.
Conor McGregor akishushia ngumi nzito mpinzani wake Floyd Mayweather
3Floyd Mayweather akimtwanga konde la shavu Conor katika pambano lililofanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa Las Vegas' T-Mobile Arena
Floyd Mayweather akishangilia baada ya kumtwanga kwa Ko Conor McGregor
Floyd Mayweather (kulia), na Conor McGregor wakisomana wakati wa pambano lao leo asubuhi.
NEVADA, Marekani PAMBANO la ngumi za kulipwa kati ya Conor McGregor na Floyd Mayweather Jnr limemalizika Las Vegas, Nevada nchini Marekani, baada ya kuchelewa kuanza kwa muda wa saa moja.Floyd Mayweather Jnr ameibuka mshindi katika mchuano huo. Maelfu ya watu wamefika katika mji wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani, kushuhudia mchuano huo mkali wa ndondi, uliofanyika leo Jumapili.
Masumbwi hayo yalikuwa ya raundi 10. Awali wachanganuzi walisema kuwa Floyd Mayweather Jnr alikuwa ameanza kulemewa katika raundi tatu za mwanzo na mpinzani wake, kabla ya kujizoazoa na kuanza kumrushia makonde mazito mazito Conor McGregor, ambaye alionekana kulemewa hasa kuanzia raundi ya saba. Alishindwa kuhimili makonde mazito ya Maywheather na kushindwa kumaliza raundi ya 10.Tayari McGregor ambaye amechana chale mwilini, ni bingwa wa taji la Ultimate Fighting- mchezo ambao mwanandondi anatumia mbinu zote za upiganaji, akitumia makonde na mateke. Lakini nyota huyo wa miaka 29, hawajawahi kushiriki mchuano wa makonde ya kulipwa- Huku May-weather mwenye umri wa miaka 40 akitajwa kuwa mpinzani wake hatari zaidi katika masumbwi.Mayweather, alikuwa akitajwa kushinda mchuano huo, huku akiahidiwa dola milioni 100, wakati wake McGregor, akiahidiwa dola milioni 30. Dola milioni 600 zinatazamiwa kupatikana kutokana na mauzo ya moja kwa moja ya tiketi za kushuhudia makonde hayo, huku mamilioni ya watu duniani wakishuhudia kupitia televisheni zao na mitandao.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment