Mbunge Esther Bulaya apata ahueni Hospilini, awashukuru wapiga kura wake.. #share
TAARIFA KWA UMMA JUU YA HALI YA MH. MBUNGE ESTER A. BULAYA
Waananchi wapendwa wa Jimbo la Bunda Mjini sambamba na watanzania wote nyote kwa umoja wenu nichukue fursa hii kuwashukru kwa maombi yenu kwa Mbunge wetu Mh. Ester A. Bulaya
Ifahamike kuwa alipatwa na tatizo katika njia ya kupumua baada kukoswa hewa ya kutosha na safi kwa muda mrefu akiwa rumande mjini Tarime ikiwa ni pamoja na pressure.
Hali ya Mhe Mbunge inaendelea vizuri na Kipekee kabisa anawashukuru wananchi Jimbo la Bunda Mjini na Watanzania kwa maombi yenu ambayo yamempa nafuu kubwa.
Kwa sasa bado yuko chini ya uangalizi wa mwisho wa madaktari wake kabla ya kuruhusiwa kuendelea na kazi zake.
Kaunya yohana
Katibu ofisi ya Mbunge jimbo la Bunda mjini



No comments:
Post a Comment