gOOD nEWS: Tecno waja na mbinu mpya kuibua na kusaidia vijana wenye vipaji mtandaoni...#share
SIMU ya Tecno imezindua kampeni ya ‘Washa cheche’ itakayodumu
kwa mwezi mmoja yenye lengo la kuibua vijana wenye vipaji vya Sanaa na
kuwasaidia kuviendeleza ili kutimiza ndoto na maleongo yao.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhusiano
wa Tecno Eric Mkomoya akizungumza na waandishi wa habari wakati wakumkabidhi
toleo jipya la Simu ya Tecno ‘Tecno Spark’ mchekeshaji Raymond Msengi.
“Nia na madhumuni ya
Kampuni yetu kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania kupitia simu hii mpya,
vijanawanaotaka kufanikiwa wanapitia vikwazo vingi ila Tecno inataka kuwasaidia
kupitia washa cheche,” alisema Mkomoya.
Amesema Msengi ambaye ni mchekeshaji wa mtandaoni aliomba
simu kutoka Tecno Mobile kupitia video zake ili aweze kurekodi kwa ubora mzuri.
Tecno Mobile walisikia kilio chake na kumpa zawadi ya simu kwa mwaka mzima kila
toleo.
Msengi amewataka vijana wengine kuthubutu kushiriki katika
kampeni hiyo kwani inaweza kuwa bahati yao na kupata zawadi hiyo.
“Nimefurahi kupata zawadi ya simu hii, na kikubwa ni kupata
mfululizo wa matoleo yote mapya ya simu zao, nawasihi vijana wenzangu wenye
vipaji wawashe cheche zao na wanaweza kupata msaada kutoka Tecno Mobile,”
alisema Msengi.
Meneja wa Masoko Mtandaoni Kelvin Boniface amesema jinsi ya
kushiriki katika shindano hilo ni kuweka picha au kipande cha video kwenye
mitandao ya kijamii ukitumia hashtag #washacheche na kisha kutag ‘Tecno Mobile
Tanzania kwenye mitandao yao ya Facebook, Twitter na Instagram.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment