GUMZO: Buda kajiua baada ya kura za Boss wake kutotosha kwenye nafasi ya Ugavana Nchini Kenya.. #share
Wahenge wetu husema... Siasa ni 'mchezo wa rafu'.. Maneno haya ya Wahenga yalithibiti jana Nchini kenya baada ya Bwana mmoja wa makamo kuamua kujimaliza mwenyewe kufuatia kushindwa Uchaguzi kwa mtu aliemtegemea sana kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Taarifa iliyochapishwa na Mkuu wa Polisi Wilayani Nyandaruwa nchini humo Kamishna Msaidizi
Timon Odingo, mwendazake huyo David Mathenge, mwenye umri wa miaka 51,.. aliacha ujumbe wa maandishi ukielezea sababu kuu ya kujiua kwake kuwa ni hali kutamaushwa kulikotokana na Gavana wa Leikipia MHE.Joshua Irungu kupoteza kiti chake, licha ya kampeni kubwa waliyoifanya..
Kumerikuwa na visa na mikasa Nchini kenya tokea Kamishna mkuu wa Tume inayosimamia Uchaguzi na Mipaka Bw. Ezra Chiloba kutangaza matokeo yualiyomuonyesha Bw. Uhuru Kenyatta akimtupa mbali mpinzani wake mkuu Bw. Raila Odinga katika matokeo ya mwisho ya kura za urais.
No comments:
Post a Comment