GUMZO Kispoti: Ona sasa 'Community Shield' ilivyozima ndoto za kuishi kwa shabiki huyu wa Haruna Niyonzima.. #share

Stori ilikuwa hivi; ndani ya "kibanda umiza" mechi ya derby jana kati ya Simba SC na Yanga SC wakati wa mikwaju ya penati alipoenda kupiga Haruna Niyonzima, Shabiki wa yanga akamwambia shabiki huyu wa simba ;

"huyu hapati hii penati ametokea kwetu Yanga"

 Pastory  akamjibu " anapata usibishe"

Niyonzima akazamisha nyavuni ule mkwaju wa penati kwa pigo zuri tu. Pastory wa simba ile furaha akapata mshituko akapoteza fahamu na kukimbizwa hospitali lakini hakuweza kuamka tena. Kutokana na ile furaha ndio ikawa mwisho wa uhai wake Rest in Peace Pastory Kigia (43yrs) Morogoro(Kilombero).


Hakika kazi ya Mungu haina makosa lakini ndugu zangu wapenda soka tuwe na kiasi katika mapenzi yetu katika mchezo huu pia lolote lile la kidunia. Ni vyema zaidi kiimani kumpenda Mungu kuliko jambo lolote . Haya mambo ya watu kufariki viwanjani na katika mabishano ya kisoka yameanza kukua kwa kasi sana sasa hivi pia watu kuzimia viwanjani. Kabla ya jambo lolote likiwepo hili la kuupenda mchezo huu ni lazima kumweka Mungu mbele akupe ustahimilivu ili uwe na yamini pia kiasi .

Hakuna aijuaye njia yake ya kuondoka humu ulimwenguni lakini tujikite zaidi kwa mapenzi ya asilimia 100/100 katika masuala ya kiimani zaidi pia tujijenge kukubali matokeo ya aina zote katika soka

Pole wana msimbazi wote , familia ya bwana Pastory , wapenda soka na wote tulioguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine- Na Samwel Samwel
INASIKITISHA SANA PUMZIKA KWA AMANI PASTORY

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search