GUMZO: Ya Zitto Kabwe 'kumwaga mchozi '.. kisa ? Tundu Lissu 'kuswekwa ndani'.. "Sijashiriki 'tala-taka'..".. mnataka Mbunge ataje 'makosa ya Rais' chooni? Chumbani? Shimoni ?.. #share

Suala la Ndege yetu kuzuiwa Canada lisifanywe Ni suala la ushabiki Kama ushabiki wa mpira. Ni suala la Nchi hili na mjadala wake uwe na hadhi hiyo. 
Kitendo cha Msemaji wa Serikali kulaumu wanasiasa Kwa jambo la kisheria Kama hili ni utoto. Hakuna mwanasiasa anayeweza kushirikiana na kampuni za kigeni kuhujumu nchi. Mimi binafsi filosofia yangu ni rahisi Sana ' My Country, Right or Wrong '. Maneno yanayosambazwa kuwa nimeshiriki kuwezesha Ndege ya Bombardier iliyonunuliwa na Serikali Kwa niaba ya ATCL kukamatwa huko Canada ni takataka tu zinazosambazwa na wapika propaganda. 


Serikali lazima ifahamu kuwa ni lazima ihojiwe na iwe tayari kutoa majibu. Sisi kama vyama vilivyo Nje ya Serikali Ni wajibu wetu kuhoji jambo lolote. Pia ni haki yetu kupata Taarifa zozote kutoka mahala popote zitakazosaidia kuisimamia Serikali. Wajibu wa Serikali ni kujibu hoja zinazoibuliwa. Majibu ya Msemaji wa Serikali yanataka kuligeuza suala hili kuwa la kisiasa na watu wameangukia kwenye ushabiki huo. Hili ni suala la kisheria na suala la nchi ambayo sisi wote tuna maslahi ya kuona inakwenda mbele. 

Nchi kudaiwa sio dhambi. Hata mataifa makubwa duniani yanadaiwa. Watu binafsi tunadaiwa sembuse Serikali? Mimi ninadaiwa madeni ya uchaguzi mpaka Sasa na wengine wamenipeleka mahakamani. Sio dhambi kudaiwa. Muhimu ni 1) Deni limetokana na Nini? Ni maamuzi mabovu ya kisiasa? 2) unalipa deni hilo au kuweka mikakati ya kulipa? 

Serikali yetu inafahamu kuwa nchi yetu Ina madeni mengi na miongoni Mwa madeni hayo yameshaamuliwa na Mahakama. Kinachopaswa ni kuwa na MAARIFA ya kupita ili kuzuia Mali zetu nje kuzuiwa Kama ilivyo Kwa Ndege Hii. Serikali iwe wazi kuhusu suala hili la Ndege. Je ile ya Boeing ( Terrible Teen ) ipo salama? Madeni mengine yenye amri ya mahakama ni yepi? Kwanini Serikali inasubiri kuhojiwa Ndio itoe Taarifa? 

Hii ni nchi yetu sote. Hakuna mwenye hatimiliki ya ukweli. Ukweli pia haupendi kupindwa pindwa. Serikali itoke kueleza nini kimetokea mpaka Ndege kuzuiwa, iachane na tabia ya hovyo ya kutafuta mchawi ' kwamba eti wanasiasa Ndio wamesababisha '. Kutafuta mchawi ni kutowajibika Kwa maamuzi ya Serikali yenyewe..
...akamalizia Zitto Kabwe: Bei ya Ndege moja aina ya Bombadier Q400 ambazo Tanzania ina/menunua ni USD 31m. Deni tunalodaiwa pamoja na riba ambalo Serikali imekiri na kuahidi kulipa ni USD 37m. 

Hivyo Serikali yetu ingeweza kununua Ndege nyengine mpya iwapo ingeshughulikia vema kesi ya kampuni iliyoshikilia Ndege yetu. Hasara za namna hii ndio hurudisha nyuma Serikali za Afrika kwenye juhudi za Maendeleo. 

Jambo la kushangaza ni pale Mbunge mwenye mamlaka ya Kikatiba kuihoji Serikali anapotimiza wajibu wake anakamatwa na kushtakiwa Kwa ' kutaja makosa ya Rais hadharani. Sasa Mbunge ataje makosa ya Rais chooni? Chumbani? Shimoni? Mbunge wa Upinzani ni lazima ataje HADHARANI makosa ya Kiongozi wa Serikali ya Chama kinachoongoza dola. 
Kazi ya Upinzani ni kuhoji. Ni kazi ya kimantiki na ya kikatiba.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search