KENYA: MSIMAMIZI WA UCHAGUZI AKUTWA AMEUAWA BAADA YA KUBAKWA...

Aliyekuwa msimamizi msaidizi wa wa tume huru ya uchaguzi IEBC katika uchaguzi mkuu nchini Kenya Kaunti ya Siaya, Caroline Odinga amekutwa amefariki dunia huku Jeshi la Polisi likisema kuwa upelelezi unafanyika wa kubaini wahusika wa tukio hilo.

Mwili wa mwanamke huyo ulikutwa katika soko la Sega Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando katika kijiji cha Lifunga.

Aidha, Mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema kuwa uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kujeruhiwa vibaya.
Hata hivyo, Familia ya marehemu huyo imesema kuwa mara ya mwisho marehemu alitoka nyumbani akielekea kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi katika Uchaguzi Mkuu ulioisha.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search