sPORTS nEWS: StarTimes RBA yaja na All Star wiki hii....#share

KAMPUNI ya StarMedia Tanzania Limited ambao ni Wadhamini Wakuu wa ligi ya kikapu ya RBA, wanataarajia kuleta mechi ya All Star mwishoni mwa wiki hii ambayo itashirikisha wachezaji vinara katika ligi hiyo.


Taarifa iliyotumwa leo kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mahusiano cha Kampuni hiyo kilibainisha kuwa mechi hiyo  inatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi Septemba 2 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imesema kuwa baada ya kuanza kwa hatua ya robo fainali (playoffs), wapenzi wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam na Tanzania Kwa ujumla watapata nafasi ya kushuhudia wachezaji vinara wa ligi hiyo wakiwapatia burudani  kupitia mchezo huo.

Mchezo utahusisha timu mbili ambazo zimepewa majina ya NYOTA na MAMBO, majina ya vifurushi vya gharama nafuu vya StarTimes, ndizo zitashuka dimbani katika uwanja wa Ndani wa Taifa ili kutoa Burudani ya aina yake kwa watazamaji.

Mchezo unatarajiwa kupigwa kati ya saa 2 hadi saa 4 Usiku, Lakini kabla ya mchezo kuanza kutakuwa na michezo kadhaa ya utangulizi na Onyesho kutoka kwa Msanii Jay Moe.

Mchezo wa All Star ni sehemu ya ufunguzi kwa hatua ya Mtoano (PlayOffs) ambayo itahusisha jumla ya timu nane (8), ili kumpata mshindi na timu tatu (3) zitakazopata nafasi ya kushiriki ligi ya Taifa hapo baadaye mwaka huu. Hatua hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 6 Septemba.

Akizungumzia muendelezo wa ligi hiyo Meneja Mahusiano wa Kampuni ya StarTimes, Juma Suluhu amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kusaidia ukuaji wa michezo nchini ikiwa ni sehemu ya Uhusiano mzuri kati ya kampuni hiyo na Watanzania.

“Tunajisikia fahari kuchangia kuinua vipaji kwa vijana wa kitanzania kupitia mpira wa kikapu ambao pia una wapenzi na washiriki wengi hivyo udhamini wetu unakuwa ni sehemu ya shughuli nyingi za kijamii ambazo kampuni yetu inaendelea kufanya” alisema Juma.

Ligi ya StarTimes RBA inaonyeshwa MUBASHARA kila siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia Chaneli ya Sibuka Maisha ambayo inapatikana katika king’amuzi cha Startimes, kwa gharama ya Tshs 3000 kwa Mwezi.

Mbali na ligi RBA StarTimes ndiyo kampuni yenye kibali cha kuonyesha michuano ya Mpira wa kikapu Kimataifa (FIBA), na sasa wanaendelea kuonyesha ligi ya Kikapu kwa Wanawake AfroBasket inayochezwa nchini Mali.
Na Abraham Ntambara


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search