Kutoka Mahakama ya Kisutu Leo: Ushahidi wa msokoto wa bhangi kesi ya Wema Sepetu bado kizungumkuti.. Mahakama ‘yajivuta’ kutoa maamuzi.. #share
MAHAKAM ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kutoa uamuzi iwapo
itapokea au kutopokea kielelezo cha ushahidi cha msokoto mmoja wa bangi
na vipisi viwili vya bangi katika kesi inayomkabili Wema Sepetu hadi mwishoni mwa
mwezi huu.
Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema uamuzi huo ulipaswa
autoe leo, lakini bado kuna tafiti anazifanya, hajakamilisha hivyo aliuahirisha
hadi Agosti 31,2017.
Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa uamuzi huo shahidi wa
kwanza wa upande wa mashtaka ataendelea kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Kesi
hiyo itaendelea kusikilizwa Septemba 12 na 13, 2017.
Uamuzi huo umefuatia baada ya shahidi huyo ambaye ni mkemia
kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima ambaye alipima msokoto
mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni
bangi, kuomba kuvitoa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.
Mulima kupitia wakili wa Serikali, Costantine Kakula aliomba
kuitoa bahasha iliyofungwa juu yenye muhuri, saini ya shahidi huyo na namba ya
maabara 291 ya 2017 ambayo ndani yake kulikuwa na msokoto na vipisi
viwili vya bangi mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.
Hata hivyo wakili wa Wema, Tundu Lissu alipinga kisipokewe
kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya
msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.
Kutokana na hoja hizo, Hakimu Simba alisema Agosti 18, 2017
atatoa uamuzi juu ya hoja hizo na kesi hiyo pia inaendelea kusikilizwa kwa
ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
N
No comments:
Post a Comment