Kutoka Mahakama Kuu: Profesa Lipumba na Kundi lake wakwaa kisiki cha ruzuku, Jaji awapiga chini...#share
MWENYEKITI wa Chama cha
Wananchi CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa
Ibrahim Lipumba na kundi lake wamekwama mahakamani leo baada ya Jaji
Ndyansobera kukataa maombi yake na kundi lake.
Jaji
Ndyansobera amekataa kufuta kesi Namba 28/2017 kama ilivyoombwa na Lipumba ili
wapate Ruzuku ya Chama Cha Wananchi wa CUF inayofikia shilingi billion
moja na million mia nne toka Julai mwaka jana.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande amesema kwamba
kufuatia uamuzi huo wa mahakama, Profesa Lipumba hataweza kuchukua haa shilingi
moja.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment