LHRC yaitaka Serikali 'kukazia macho' vitendo vya uminywaji Wa Haki za kisiasa na kiraia nchini.. #share

KUTUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeitaka Serikali kuwajibika haraka iwezekanavyo kuchukua hatua stahiki za kisheria ili kulinda na kutetea haki ya watanzania walio wanyonge, isipofanya hivyo wao watachukua majukumu hayo.


Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Wa Utetezi na Maboresho wa LHRC Anna Henga, amesema kituo hicho kinasikitishwa kuona vitendo vya uminywaji Wa Haki za kisiasa na kiraia nchini.
" Hali hii imejitokeza sana kwa kuwanyanyasa wabunge wa Vyama vya upinzani, kamata kamata kwa viongozi hao imeebdelea bila kufuata misingi ya sheria na haki za binadamu katika ukamataji huo," amesema Henga.
Ametaja baadhi ya wanasiasa waliokamatwa bila kufuata misingi hiyo ya sheria kuwa ni pamoja na Tundu Lissu ambaye bado anakesi mahakamani, Ester Bulaya na Godbless Lema aliyekamatwa jana akituhumiwa kuzidisha muda wa mkutano kwa dakika saba.
Aidha amesema kituo hicho kimepokea baadhi ya matukio mengine ya uvunjifu wa haki za binadamu kama migogoro ya ardhi kati ya serikali na wananchi, TANAPA dhidi ya wananchi walio jirani na hifadhihifadhi, Askari kuua wananchi na Mgogoro wa TANROAD na wananchi.
Ameeleza kuwa kutokana na Matukio hususana yanayotendwa na askari wamependekeza kutolewa kwa mafunzo maalumu kwa askari ili kujua jinsi ya kutekeleza majukumu yao bila kuathiri Haki za wananchi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search