Maneno ya Ommy Dimpoz yawavuruga akina Platnumz.. Esma aja na neno zito... #share

Dada wa mwimbaji Diamond Platnumz, Esma Platnumz ni miongoni mwa watu walioguswa na pengine kuumizwa na ujumbe wa Ommy Dimpoz kupost picha akiwa na mama yao na kuandika maneno ambayo hayajamfurahisha baada ya kutokea beef baina yake na Diamond Platnumz.
Katika post hiyo ya Ommy Dimpoz, Esma aliweka comment ambayo ilikuwa onyo kwa staa huyo wa ‘Cheche’ akimwambia aache kumhusisha mama yake na ugomvi wake na Diamond.

Esma alicomment:>>>“Maugonvi yenu msimuingize na mama yangu plz kuwa na adabu tukaneni wenyewe but siyo mama yangu jiheshimu naona sasa unazid” – Esmaplatnumz...Kumekua na vijembe vya hapa na pale kati ya pande mbili za Bongofleva, Diamond Platnumz na WCB na Alikiba na Rock Star ambapo ishu imeanzia kwenye fresh remix ya Fid Q ft. Diamond na Rayvanny.... Millardayo.
-------------

Alikiba alijibu kupitia ukurasa wake wa Twitter na Instagram ambapo saa kadhaa baadae kuna kipisi kingine cha hiyo ngoma ya Fresh kilipostiwa Instagram na Diamond alisikika akichana maneno yafuatayo hapa chini.
Kufanya verse moja tu naona povu linawashuka, kina dada wavaa top na vibukta.. hawatoi ngoma kazi Twitter kunisuta
Mistari hiyo ilisemekana kumdiss Alikiba na Dimpoz ambapo Ommy Dimpoz leo ametumia ukurasa wake wa Instagram kupost picha akiwa na Mama mzazi wa Diamond Platnumz na kuandika “BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU, Salam zako nimezipata mwanangu”
Hivi kweli ww wa kukosa Adabu na kuamua kunichamba mimi Baba yako? Sasa kosa langu mimi nini? Kwani kuna Ubaya kumtandikia Kitanda Baby wako King?”



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search