mAHAKAMANI kISUTU: Kesi ya Aveva na Kaburu yatajwa na kuahirishwa..... Warudisha rumande hadi Septemba 8 mwaka huu...#share

VIONGOZI wa klabu ya Simba, Rais Evans Aveva na Makamu wake,
Geoffrey Nyange maarufu kama Kaburu imetajwa na kuahirishwa kwa mara ya
saba, huku ikipangwa kusikilizwa tena Septemba 8, mwaka huu.
Evans Aveva (kushoto) na MGeoffrey Nyange 'Kaburu'
Victoria Nongwa ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu,
Dar es Salaam anasikiliza kesi hiyo amesema ameiahirisha kesi hiyo ili
kupisha uchunguzi wa nyaraka zilizokusanywa.
Hata hivyo, Hakimu Nongwa amewataka mawakili wa upande wa
Serikali kuharakisha kufuatilia nyaraka za vielelezo zilizokusanywa ili kesi
hiyo ianze kusikilizwa.
Wawili hao wanakabiliwa na mashitaka matano, yaliyofunguliwa
na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), yakiwemo ya utakatishaji
fedha, ambayo hayana dhamana na wote wapo rumande gereza la Keko tangu Juni 29,
mwaka huu.
Aveva na Kaburu wanadaiwa kughushi nyaraka zinazoonesha
Simba inawalipa madeni kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 (zaidi ya
shilingi milioni 672).
Inadaiwa Aveva alitoa nyaraka za uongo kwa Benki ya
CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni
kutakatisha fedha kinyume cha sheria, yeye na Kaburu walikula njama za kufanya
uhalifu huo.
Shitaka la nne linamhusu Kaburu kutakatisha dola 300,000 na
kuziweka katika Benki ya Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam,
na la tano ni kutakatisha fedha yeye, na kumsaidia Aveva kufanya hivyo katika
benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.
Na Mwanadishi Wetu
No comments:
Post a Comment