MATUKIO PICHANI: WALLACE Karia aapishwa kuwa Rais wa TFF, aahidi kuanika Taarifa ya Mapato na Matumizi kwenye Magazeti... #share



Pix 1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Michael Wambura (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa TFF uliofanyika leo katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma
Pix 2
: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia (kulia) akiapa mbele ya Wakili na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini Bw. Ibrahimu Mkwawa (aliyesimama kushoto) baada ya kutangaza mshindi wa nafasi hiyo leo katika Ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma
Pix 3
Mwakilishi wa TFF kutoka zoni namba nne Bi. Sarah Chao (kulia) akiweka sahihi katika kiapo alichoapa baada ya kutangaza mshindi leo wakati wa Mkutano Mkuu wa TFF Mkoani Dodoma. Kushoto aliyesimama ni Wakili na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini Bw. Ibrahimu Mkwawa
Pix 4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya hiyo Pro. Elisante Ole Gabriel (katikati) wakifuatilia uapisho wa viongozi wapya wa TFF waliochagulia leo katika Mkutano Mkuu wa TFF Mkoani Dodoma
Pix 5
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa TFF (hawapo pichani) baada ya kutangazwa na kuapishwa kwa viongozi wapya wa TFF leo Mkoani Dodoma. 
Pix 6
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF kumwezesha kushika nafasi ya urais leo wakati wa Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika katika Ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM
………………………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Uongozi mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umetakiwa kufikia Januari mwakani kuwajibika kama mashirika mengine ya mpira wa miguu duniani yanavyowajibika kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wapate fursa ya kufahamu namna fedha zinavyopatikana na jinsi zinavyotumika katika kuboresha  na kuendeleza usimamizi bora wa soka nchini.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na leo katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma
Aidha Mhe. Mwakyembe amewapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne kwa kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku huku akiwapongeza washiriki wote waliothubutu kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF wa mwaka huu.
Kwa upande wake Rais mpya wa TFF Bw. Wallace Karia amewaahidi wapiga kuwa wake kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwani nafasi aliyopewa na wajumbe hao kwa kumuamini ni deni ambalo atalilipa kwa kuleta mafanikio makubwa katika mchezo wa soka.
Bw. Karia amesema kuwa furaha waliyonayo viongozi wote waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne iende kuwa furaha ya kazi kwa kufanya yale watanzania wanatarajia kutoka kwao.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search