Meya Mwita wa Ukawa 'aitolea macho' Bilioni 40 ya NSSF ndani ya Machinga Complex.. amtaka Waziri Simbachawene kuingilia kati.. #share

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam limemuomba waziri  nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, George Simbachawene kuingilia mgogoro uliopo katiya Jiji hilo na mfuko wa hifadi ya jamii (NSFF)  katika jengo la Dar es Salaam City Council Business Park  (Machinga Complex) kutokana na jiji hilo kutakiwa kulipa Bilioni 40  kinyume na mkataba.


Pia jiji hilo limesema wako tayari kulikabidhi jengo hilo kwa NSSF ili wao waliendeshe  ili waweze kurejesha  fedha  zilizotolewa na mfuko huo kama mkopo kwa halmashauri ya jiji  ya ujenzi wa jengo hilo kutokana na jiji hilo kushindwa kulipa deni hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Meya wa Jiji hilo, Isaya Mwita amesema wamefiia hatua hiyo ya kuwataka viongozi wa serikalini pamoja na kurudisha jengo hilo kutokana na kutorizika na hatua ya NSSF kuwataka walipe bilioni 40 tofautisha na mkataba  unavyotaka.

"Jiji la   halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ilingia mkataba  na NSSF  wa mkopo wa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi  wa jengo hili mkataba huu ulifanyiwa nyongeza ya bilioni 12.45  na kufanya mkopo ambao tunadaiwa ni bilioni 12.45,''

''lakini makabidhiano  ya jengo yalifanyika mwaka 2010 garama jengo ilikuwa ni Bilioni  12.7 kwa  sasa kwamba eti deni hilo linaladaliwa kuwa zaidi ya bilioni 40"amesema Mwita.

Mwita ambaye ni meya wa anayeungwa mkono na Vyama vinavyounda ukawa amesema Halmashauri ya jiji hilo imebaini pia kuna ukiukwaji mkubwa wa kimkataba katika jengo hilo kwakuwa mkataba unalitaka jengo hilo liwe na vizimba elfu kumi lakini badala yake limekuwa na vizimba elfu nne tu  huko gorofa  ilitakiwa kuwa na gorofa tano upande mmoja na ghorofa  sita upande mwingine  lakini  wamepewa jengo lenye gorofa nne kinyume na mkataba.

Mwita amebainisha kuwa  Halmashauri hiyo haikuhusika na usimamizi wa fedha wa fedha  zilizokopwa  na kuifanya  kushindwa  kuthibitisha gharama  zilizotumika .

"Mkataba ulitaka  NSSF  kutoa fedha  kwa Halmashauri  ya Jiji kwa ajili ya ujenzi  wa jengo hilo jambo ambalo halikufanyika ,huku fedha zilizoongezeka kutoka shilingi bilioni 12.14  hadi kufukia shilingi Bilioni 12.7 ziliongezwa bila kufikia  makubaliano yoyote  kaika halamshauri na NSSF."ameongeza kusema Mwita.

Aidha Mwita amesema licha ya Halmashauri hiyo kwa muda mrefu  imekuwa ikijaribu  kutafuta muafaka  na NSSF wa ulipaji deni hilo bila mafanikio .

"Kwa kutambua  umuhimu wa urejeshaji wa fedha hizo zinazotakanwa  na michango ya wanachama wa mfuko huo na kwa kuzigatia  hali halmahsauri ya jiji tumebaini halilipiki,''

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search