nEWS: TIC yavunja rekodi usajili miradi ya uwekezaji, pia ya zalisha ajira kwa watanzania....#share
KITUO cha Uwekezaji (TIC) kimesajili hadi sasa miradi 209 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu ambayo
inategemewa kuzalisha ajira rasimi na zisizo rasmi zaidi ya 12,452.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji
wa TIC Geofrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari, alisema kiwango hicho
ni kikubwa ukilinganisha na mwaka uliopita ambapo walisajili miradi 306 tu.
“Hadi sasa tumekwisha sajili miradi 206 kwa kipindi
cha miezi saba, hii inamana kwamba tunaeza kusajili miradi mingi zaidi kwa muda
huu uliobaki kabla ya mwaka huu kumalizika,” alisema Mwambe.
Aidha alisema wameandaa mpango maalum wa Mfuko wa
Benki ya Ardhi ambao utasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa ardhi na kuleta ufanisi katika upatikanaji wa maeneo
ya ujenzi wa viwanda pamoja na uwekezaji mwingine.
Alisema hadi sasa maeneo yaliyopatikana kwa ajili ya
ujenzi wa viwanda ni Kigamboni na Tanga na wanategemea kuongezeka kwa mitaji ya
kutoka nje na ndani yaani FDI na DD1 kutokana na kupata miradi mikubwa Sita.
Mwambe alifafanua kuwa miradi hiyo yenye hadhi ya
kimkakati iliyosajiliwa na TIC na kupitishwa na Baraza la Taifa la uwekezaji.
alisema miradi hiyo kwa pamoja inategemewa kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani
sh. bilioni 2.626 na inatarajiwa kuzalisha
kiasi cha ajira 13,885 ambazo zitanufaisha watanzania.
alieleza kuwa juhudi za uhamasishaji ujenzi wa viwanda
zimeweza kuzaa matunda na mpaka sasa wameweza kusajili viwanda vikubwa ambavyo
vitasaidia katika kubadilisha hali ya uchumi wa nchi.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment