nEWS: Mahakamani Kisutu, Waanzilishi wa Jamii FORUMS wakana mashtaka dhidi yao......#share
MKURUGENZI wa Kampuni ya Jamii Media Limited, Maxence
Melo na mmiliki mwenza wa kampuni hiyo Mike William leo Mahakamani Kisutu wamekana maelezo
waliyosomewa ya kulizuia Jeshi la Polisi kuuchunguza mtandao huo.
Melo na William wamekana hayo baada ya kusomewa maelezo ya
awali na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Godfrey Mwambapa katika
kesi ya kulizuia Jeshi la Polisi kuuchunguza mtandao wao kwa kuchapisha taarifa
za uongo.
Katika maelezo hayo, Melo na William wamekubali
wasifu wao, ikiwemo majina, umri, kumiliki mtandao wa Jamii Forum na kukamatwa kisha
kufikishwa Mahakamani lakini hata hivyo, wamekana kuhusika na tuhuma za
kulizuia Jeshi la Polisi kuuchunguza mtandao huo.
Baada ya kusomewa maelezo hayo,
Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo
hadi August 24, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Katika kesi hiyo inadaiwa Melo na William walizuia
Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya
Makosa ya Mtandao huku ikidaiwa kati ya May 10 na December 13, 2016 maeneo
ya Mikocheni, Kinondoni, walilizuia Jeshi hilo kufanya uchunguzi baada ya
kuchapishwa taarifa za uongo dhidi ya kampuni ya CUSNA Investment na Ocean Link.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment