nEWS nAIROBI kENYA: Odinga avaa kofia ya Kenyatta, atangaza kesho siku ya mapumziko nchi nzima...#share
ALIYEKUWA mngombea wa kiti cha Urais nchini Kenya kwa tiketi
ya Muungano wa Vyma vya Upinzani (NASA) amatangaza kesho kuwa siku ya mapumziko
nchi nzima.
Ametoa kauli hiyo mapema leo akizungumza na wafuasi wa NASA
wakati akitoa salamu za lambalambi kwa familia iliyofiwa na mtoto wao Moraa
Nyaranga (10).
NASA wamedai kuwa mtoto huyo ameuawa kwa kupigwa risasi jana
na askari polisi.
Tangu kutangazwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa Urais kwa
awamu ya pili nchini Kenya, kumekuwa na maandamano ya wafuasi wa NASA wakidai
kuibiwa kura hali ambayo imepelekewa kuwa na makabiliano baina ya polisi na
waandamanaji.
Aidha kauli hiyo imekuja kukiwa na taarifa kwenye baadhi ya
mtandao nchini Kenya zinadai hadi leo zaidi ya wananchi 20 wamepoteza maisha
katika maeneo mbalimbali nchini humo kutokana na kuzuka kwa ghasia za kupinga
matokeo ya uchaguzi huo.
Alhamisi iliyopita, NASA ilidai Odinga ndiye aliyeshinda
uchaguzi huo na kuitaka IEBC kumtangaza kuwa mshindi.
Katika uchaguzi huo Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290
ambazo ni asilimia 54.27 huku Odinga akapata kura milioni 6,762,224 sawa na
asilimia 44.74.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment