tREANDING nEWS: Kofi Annan ampa mbinu Odinga kuingia IKULU Kenya...#share
KATIBU Mkuu wa zamani
wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan, ametoa wito kwa muungano wa vyama vilivyoshindwa
kwenye Uchaguzi Mkuu nchini humo kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki.
Annan alikuwa mpatanishi
mkuu wa mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, baada ya ghasia
kuzuka kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2007 uliokumbwa na utata ambapo Rais mstaafu Mwai
Kibaki alitangazwa mshindi wakati huo huku Raila Odinga na chama chake cha ODM na
muungano wa vyama vya NASA wakapinga matokeo hayo.
Katika taarifa yake
Annan amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa ushindi huku akamsifu kiongozi wa
NASA, vinavyolalamikia hujuma kwenye uchaguzi huo, kwa kuendesha kampeni yake
kwa njia ya amani.
"Namshukuru kiongozi
wa upinzani Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi
jasiri wa demokrasia," alisema Annan kupitia taarifa yake.
Ameongeza: "Hivyo,
namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa
na aweke maslahi ya taifa mbele, kama alivyofanya awali kwa uzalendo na mara
nyingi,”
Annan amesema upinzani
umekuwa ukidai mitambo ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ilidukuliwa
na matokeo kuchakachuliwa ili kumpa ushindi Rais Kenyatta.
Wakati Annan akitoa rai
hiyo kwa NASA taarifa za baadhi ya mtandao nchini Kenya zinadai hadi leo zaidi
ya wananchi 20 wamepoteza maisha katika maeneo mbalimbali nchini humo kutokana
na kuzuka kwa ghasia za kupinga matokeo ya uchaguzi huo wa Agosti nane.
Alhamisi iliyopita, NASA
ilidai Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na kuitaka IEBC kumtangaza kuwa
mshindi.
Katika uchaguzi huo Rais
Kenyatta alipata kura 8, 203, 290 ambazo ni asilimia 54.27 huku Odinga akapata
kura milioni 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.
Mawakala wakuu wa NASA
waliondoka ghafla katika kikao cha tume hiyo cha kuafikiana kuhusu matokeo hayo
kabla ya kutangazwa kwa Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment