nEWS: Rais wa TLS Tundu Lissu awashambulia vikali Mawakili waliopuuza Mgomo wa kutokwenda Mahakamani leo na kesho...Atoa kauli nzito dhidi yao...#share

RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Tundu Lissu, amesema mawakili waliokwenda katika Mahakama na Mabaraza ya aina zote kutekeleza majukumu yao ya uwakili ni ishara kuwa wanaunga mkono utawala wa mabomu nchini.



Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya Tamko la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) la kukemea na kulaana shambulio dhidi ya Ofisi za IMMMA Advocates lililotokea hivi karibuni.

Aidha amesema kuwa mawakili hao watakuwa hawaungi mkono jitihada za kuhakikisha kunakuwepo usalama wa mawakili katika kutekeleza majukumu yao ya uwakili.

“watakuwa wanasema kwamba ni sawasawa ofisi za mawakili kupigwa mabom, watakuwa wanasema ni sawasawa kwa mawakili kushambuliwa, watakuwa wanasema kwamba ni sawasawa kwa mawakili kupotea,” amesema Lissu.

Amebainisha tamko la kususia kuhudhuria mahakamani na kwenye mabaraza ya aina zote kwa siku mbili leo na kesho walilitoa kama  viongozi waliopewa dhamana ya uongozi na mawakili nchini hivyo walidhani tukio hilo la shambulio ni kubwa la kuwafanya wapeleke ujumbe kwa jinsi hiyo.
“Kama kuna wakili anadhani kwamba tumekosea anahaki ya kuamini hivyo,” amesema Lissu.

Ameongeza kwa kusema kuwa lengo la mgomo ni huo ni kutoa ishara ya kutoukubali utawala wa mabomu nchini huku akiwataka mawakili wanaofikiri kilichotokea kuwa ni kitu cha kawaida  waendelee kudhani hivyo.

Aidha amesema baada ya mgomo huo wataendelea kufuatilia suala hilo ikiwa ni pamoja na kufanya mkutano na vyombo vya usalama ili kuwaeleza hofu waliyonayo kama  mawakili.

Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search