POLISI: Jeshi la Polisi leo limetaja sababu Tundu Lissu kupimwa mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali akiwa na kosa la uchochezi...#share

KAMADA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Lazaro Mambosasa ametaja sababu ya kumpeleka mtuhumiwa wa kesi ya  uchochezi kupimwa mkojo kwenye Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.



Hivi karibuni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Tundu Lissu, Jeshi la Polisi lilimpeleka kumpima mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali huku ikifahamika kuwa anashutumiwa kwa kosa la uchochezi.

Akizungumza leo wakati akijitambulisha kwa waandishi wa habari na wananchi wa jijini humo kama Kamanda Mpya wa Mkoa huo, amesema kuwa lengo la kumpima mkojo ni kutaka kujua kama mtu huo anafanya hayo akiwa na akili zake timamu au la.

Aidha amesema kwamba  matumizi ya vileo na dawa za kulevya vinaweza kumfanya mtu kuropoka hovyo kutokana na kwamba matumizi ya vitu hivyo huchangia mtu kupoteza au kupungua busara zake.

“Vileo vya pombe na dawa za kulevya  watumiaji wake hawako salama busara zao hupungua,” amesema Mambosasa.

Amesema kutokana na sababu hiyo mtuhumiwa wa jinsi hiyo hupelekwa kwa Mkemia kubaini iwapo anatumia moja ya vitu hivyo ili kujua kama ndiyo chanzo cha yeye kuongea lolote anapojisikia pasipo kuzingatia utaratibu.

Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search