nEWS: Shambulio dhidi ya Ofisi za Mawakili ya IMMMA Advocates latua kwa Dk. Bisimba na LHRC yake..Atoa Tamko kali dhidi ya tukio hilo..Pia aunga Mkono Mgomo wa Mawakili ulioanza leo na kesho...#share
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana
na wadau wengine wa haki za binadamu kimekemea na kulaana vikali shambulio
dhidi ya Ofisi ya Mawakili wa IMMMA
Advocates huku kikitoa
mapendekezo saba kwa serikali ili kuimarisha utawala bora nchini.
Aidha kimemshauri Rais John Magufuli kumteua Jaji Mkuu kwa
mujibu wa Katiba ili kuimarisha mhimili wa mahakama na utawala wa sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jinni Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dr. Hellen Bisimba amesema shambulio hilo linahatarisha utetezi wa haki
ya uwakilishi na uwezo wa wanasheria kutekeleza majukumu yao bila vitisho.
“Kanuni ya 16 ya Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa juu ya
Wajibu wa Wanasheria za 1990 (UN Basic Principles on the Role of Lawyers 1990)
inasema kwamba Serikali zitahakikisha kwamba wanasheria wanatekeleza majukumu
yao bila vitisho, vikwazo au kuingiliwa kinyume na sheria,”
“Pia, Kanuni hiyo inakataza wanasheria kutishiwa kushtakiwa
au kuwekewa vikwazo vya kiuchumi au kiutawala pale wanapokuwa wakitekeleza
majukumu yao ya kikazi,” alisema Bisimba.
Kufuatia tukio hilo Bisimba amesema Jumuiya ya watetezi wa
haki za binadamu imepatwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na ulinzi
wa haki za binadamu nchini, ikiwemo uminywaji wa uhuru wa wanasheria na haki ya
uwakilishi.
Kutokana na hali hiyo LHRC imetoa mapendekezo saba kwa
serikali kwa ajili ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama wa haki za binadamu
nchini. Bisimba alitaja mapendekezo hayo kuwa ni, Serikali, kupitia Jeshi la
Polisi, kuhakikisha watu ambao wamehusika na shambulio la Ofisi ya Mawakili ya
IMMMA Advocates wanakamatwa nakuchukuliwa hatua kali za kisheria haraka
iwezekanavyo.
Amesema nyingine ni Tasnia ya Sheria iachwe huru katika
kufanya kazi zake na kupatiwa ulinzi kwa mujibu wa sheria na wanasheria waachwe
watekeleze majukumu yao bila kuingiliwa wala kutishiwa.
Mahakama kama mhimili muhimu katika usimamizi wa haki, ina
wajibu wa kuhakikisha kwamba maofisa wote wanafanya kazi chini ya mhimili huo
wanakuwa salama na wanalindwa kwa mujibu wa sheria katika kutekeleza majukumu
yao.
Kumshauri Rais John Magufuli kumteua Jaji Mkuu kwa mujibu wa
Katiba, ili kuimarisha mhimili wa Mahakam na utawala wa sheria.
Mengine ni Viongozi wa serikali na vyombo vyake wenye dhamana
ya kulinda usalama wa watu nchini na haki za binadamu kwa ujumla wawajibike au
kuwajibishwa mara moja pale ambapo wameshindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao
kwani wanasikitika hadi jana kutosikia kauli rasmi ya serikali kulaani kitendo
hicho.
Aidha amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuripoti
matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu na uhalifu, ikiwemo mauaji mbalimbali
yenye utata kwa vyombo vya dola na vituo vya kutetea haki za binadamu bila
woga.
Ametoa wito kwa wananchi wote wenye mapenzi mema wakiwemo
mawakili wakemee vitendo kama hivyo kwani vinaathari kwa kila mwananchi.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment