nEWS: TABOA wamjaribu JPM.....Wagomea Mashine za Kielekroniki kukatia tiketi za Mabasi.....#share
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa TABOA, Abdalah Mohamed
tofauti hizo ni zile zinatokana na changamoto ya matumizi ya mashine za
kieletroniki ambapo ni lazima eneo husika kuwa na huduma za Internet ilihali
huduma hiyo haipatikani vizuri maeneo yote nchini hivyo ipo hatari ya watu
kushindwa kupata tiketi iwapo maeneo waliyopo hayana huduma hiyo.
Kutokana na hali hiyo wajumbe wa mkutano huo mkuu wa TABOA
wakaingia katika majadiliano makali huku baadhi wakitaka mkutano mkuu mwingine
wa dharura uitwe huku mawaziri wenye dhamana ya ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
na yule mwenye dhamana ya fedha na mipango na wasaidizi wao wawepo ili
kulijadili suala hilo na kulipatia ufumbuzi.
Hata hivyo mkutano huo ukaunga mkono hoja ya Naibu Katibu
mkuu wa TABOA, Issa Nkya ya kutolewa wiki moja kwa kamati maalum ya TABOA
ambayo ilikuwa imeundwa kufuatilia suala hilo wamalizane na mamlaka ya mapato
Tanzania -TRA kupitia kamishina mkuu wa kodi na ikishindikanika wachukue hatua
nyingine.
Na Muungwana.blog




No comments:
Post a Comment